Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbappe anavyozitafuna rekodi za Messi

Mbappe 2 Goals.jpeg Mbappe anavyozitafuna rekodi za Messi

Mon, 5 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kylian Mbappé Lottin ni mchezaji wa soka wa Ufaransa ambaye anacheza kama mshambuliaji wa klabu ya Paris Saint-Germain, PSG inayoshiriki Ligi kuu ifahamikayo kama Ligue 1 na timu ya taifa ya Ufaransa.

Anachukuliwa kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi ulimwenguni, Mbappé anasifika kwa uwezo wake wa kucheza chenga, kasi ya kipekee na umaliziaji.

Mshabuliaji huyo amedhihirisha uwezo mkubwa sana akiwa bado angali kinda (umri wa miaka 23).

Mchezaji huyo amekuwa miongoni walioleta chachu ya Ushindi na kufanya Timu yake ya Taifa isonge mbele kwa kutinga nafasi ya kushiriki Robo Fainali ya michuano hio ya Kombe la Dunia inayofanyika Nchini Qatar.

Ana jumla ya Mabao 9 ya Kombe la Dunia baada ya kushiriki Msimu wa 2 katika michuano hio. Ubora wake unaonekana kuwa ni zaidi ya magwiji kama vile Diego Maradona, Cristiano Ronaldo, Suárez, Neymar, Thierry Henry, Rivaldo, Kempes… na zaidi.

Mabao yake kwa sasa ni sawa na Lionel Messi – lakini Kombe la Dunia 3 chini ya nyota wa Argentina na bado anaweza kuwa na rekodi nzuri zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live