Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbappe amuweka kando Pele

Mbappe 2 Goals.jpeg Kylian Mbappe

Tue, 6 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kylian Mbappe amevunja rekodi ya Pele baada ya kufunga mabao tisa kwenye fainali za Kombe la Dunia akiwa na umri wa miaka 23, na kumpiku mkongwe huyo mwenye mabao saba.

Mbappe alifunga mabao mawili dhidi ya Poland na kutinga robo fainali ya Kombe la Dunia katika fainali hizo zinazoendelea huko Qatar baada ya kuifunga Poland mabao 3-1. Bao la Poland liliwekwa kimiani na Robert Lewandowski kwa mkwaju wa penalti.

Vilevile Mbappe anaifukuzia rekodi ya mkongwe wa Ujerumani, Miroslav Klose aliyefunga mabao 16 katika mechi 24 alizocheza, mkongwe huyu amecheza fainali za Kombe la Dunia kuanzia mwaka 2002, 2006, na 2010, 2004. Lakini kwa upande wa Mbappe ameanza kucheza Kombe la Dunia kuanzia mwaka 2018.

Licha ya kufikia idadi ya mabao ya Messi aliyofunga kwenye Kombe la Dunia baada ya kuvunja rekodi ya Diego Maradona, Mbappe amempiku Cristiano Ronaldo aliyefunga mabao manane wakati Messi akipachika mabao tisa.

Olivier Giroud, 36, amekuwa mfungaji bora wa Ufaransa wa muda wote baada ya kufikisha mabao 52. Straika huyo amevunja rekodi ya Thierry Henry aliyeshikiria kwa muda mrefu.

Mbappe aliisaidia timu yake kutinga roboa fainali. Sasa Ufaransa itacheza dhidi ya England baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Senegal.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live