Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbappe amshtaki muuza kababu

Mbappe X Injury Iiii Mbappe amshtaki muuza kababu

Fri, 15 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Supastaa wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe ameripotiwa kumshtaki mmiliki wa duka linalouza kababu huko Ufaransa baada ya kutumia jina lake kwenye kutangaza biashara yake hiyo.

Mohamed Henni, ndio ambaye amefungua duka hilo la kuuza kababu aina ya Klub ambazo zinatengenezwa kwa mkate wa duara ambao mwenyewe anauelezea unafanana na fuvu la kichwa cha Mbappe.

Kababu hizo zinauzwa kupitia mtandao kwa wale walio nyumbani, pia zinauzwa kwenye duka hilo.

Ripoti zinadai timu ya wanasheria wa Mbappe imemchukulia hatua za kisheria Mohamed wakiamini anachafua jina la staa huyo.

Henni, ambaye ana wafuasi milioni 1.8 kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, kupitia ukurasa wake kwenye mtandao huo aliweka picha zilizokuwa zinaonyesha barua alizopokea kutoka kwa wanasheria hao.

Barua hiyo ilionyesha kwamba imetumwa na Delphine Verheyden, mwanasheria wa Mbappe kwa niaba ya KMA, ambayo ni kampuni iliyoanzishwa kwa ajili ya kusimamia biashara na haki za picha za staa huyo.

Henni ametakiwa kuondoa jina la Mbappe kwenye menu yake ndani ya siku nane na akishindwa kufanya hivyo atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kutumia jina la staa huyo kwenye biashara bila ridhaa yake.

Hata hivyo, Henni alionekana kuipokea taarifa hiyo tofauti akisema Mbappe na wawakilishi wake wamekosa hata aibu kwa kumtumia barua hiyo.

“Nimeshangaa mchezaji mkubwa wa ngazi ya Mbappe anatenga muda wake kuanza kufikiria kuhusu mimi, anatumia muda na pesa zake kunishambulia wakati mimi sijamuumiza mtu yeyote.”

Chanzo: Mwanaspoti