Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbappe akomaa na Lionel Messi PSG

Lionel Messi And Kylian Mbappe 1140x640 Mbappe akomaa na Lionel Messi PSG

Wed, 12 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain Kylian Mbappe amesisistiza suala la kutaka kuendelea kucheza sambamaba na Mshambuliaji kutoka nchini Argentina Lionel Messi.

Messi anatajwa kuwa kwenye orodha ya wachezaji wananaotarajiwa kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu, kufatia mkataba wakekuwa ukingoni.

Tayari klabu yake ya zamani FC Barcelona inatajwa kuwa katika mawindo ya kutaka kumrejea Camp Nou, ambako mashabiki wamekuwa akitakani kumuona akivaa jezi ya klabu hiyo kwa mara nyingine.

Mbappe amekuwa katika harakati za kutaka Messi asalie klabuni hapo, ili kuendelea kutoa huduma nzuri na kuiwezesha kutwaa mataji mengi zaidi kwa misimu ijayo.

Hata hivyo Rais wa Paris Saint-Germain, Nasser Al-Khelaifi anatajwa kuwa kwa sasa yupo katika mazungumzo na Messi kuona anaendelea kusalia ndani ya kikosi hicho.

Messi alisajiliwa Paris Saint-Germain msimu wa 2021/22 kwa mkataba wa miaka miwili, akafanikiwa kutwaa taji la Ligue 1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live