Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbappe aipa ushindi PSG

France Soccer League One 83730 Mbappe aipa ushindi PSG

Thu, 29 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kylian Mbappe ameipa ushindi Paris St-Germain mbele ya Strasbourg ukiwa ni mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu nchini Ufaransa kwa mchezaji huyo baada ya kushindwa kutetea taji la Kombe la Dunia Qatar mbele Argentina.

Beki wa Brazil, Marquinhos aliwai kuwapa uongozi PSG kabla ya kujifunga tena na kufanya matokeo kuwa sare mpaka dakika za nyongeza ambapo Mbappe akikwamisha mpira nyavuni kwa njia ya penati.

Wakati PSG wakitafuta bao la uongozi walijikuta wakipoteza nguvu kazi kufuatia nyota wa kimataifa wa Brazil Neymar Jr kuonyeshwa kadi nyekundu ikifuatiwa na kadi mbili za njano.

Matokeo hayo yanaifanya PSG kuwa kileleni kwa tofauti ya pointi nane dhidi ya timu ilivyo nafasi ya pili Lens wakati hali ya Strasbourg ikiendelea kutweta.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live