Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbappe aipa mtihani PSG

Mbappe PSG 768x432 Kylian Mbappe

Wed, 22 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa michezo wa Klabu ya PSG, Leonardo amesisitiza kuwa wapo kwenye nafasi nzuri ya kuhakikisha kuwa mshambuliaji wao hatari, Kylian Mbappe anabaki klabuni licha ya kuwa mkataba wake unaisha majira ya joto.

Mbappe mwenye umri wa miaka 22, ameifungia klabu hiyo mabao 145 kwenye michezo 194 katika mashindano yote tangu aliposajiliwa mwaka 2018 akitokea klabu ya Monaco kwenye usajili uliomfanya kuwa mchezaji ghali wa pili duniani wa muda wote.

“Ni suala muhimu sababu tunazungumzia mchezaji bora wa dunia, ambaye mkataba wake unakwenda kuisha,” alisema Leonardo akinukuliwa na Jarida la France Football.

“Tunaweza kusema tumezungumza naye mara nyingi kwa njia ya upole zaidi, lakini ndio sehemu ya kujenga mahusiano.

“Kuna gumu kidogo ila kwa namna nyingine tungependa aendelee kuwapo maisha yake yote hapa na pia itatupasa kuheshimu nafasi ya familia yake, nadhani tunanafasi nzuri ya kuhakikisha anasalia hapa, naamini hilo.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live