Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbappe achoka kusikia habari za kurogwa, amvutia simu Pogba

Pogba Family Ml Mbappe achoka kusikia habari za kurogwa, amvutia simu Pogba

Sat, 3 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vyombo vya habari nchini Ufaransa vimeripoti kuwa Kylian Mbappe sasa ameonekana kuchukua hatua kwa kumpigia simu mchezaji mwenzake Paul Pogba baada ya jina lake kuingizwa kwenye ugomvi wa kifamilia ambapo kaka mkubwa wa mchezaji mwenzake wa timu ya Ufaransa Paul Pogba, Anayejulikana kama Mathias Pogba kumtaja Mbappe katika tuhuma za uchawi dhidi yake.

Mazungumzo rasmi kati ya wawili hao bado hayajafahamika lakini mshambuliaji huyo wa PSG alitaka kujua kinachoendelea baina ya wahusika wakuu wawili wa suala hili linalozidi kutapakaa kwenye vyombo vya habari ili kujua kiunagaubaga juu ya kichoendelea.

Kwa kujikumbusha tu, Paul Poaba alinukuliwa akisema Mathias Pogba ambaye ni kaka mkubwa wa Paul Pogba na rafiki zake wengine wa utotoni walimtishia mchezaji huyo wa Juventus na kumtaka awape kiasi cha pesa ili wasiweke wazi shutma za uchawi dhidi yake ambazo pia anazifanya dhidi ya Kylian Mbappe.

Siku chache zilizopita Mathias Pogba alichapisha jumbe za sauti mitandaoni ambapo amemshutumu Pogba kwa kuongea na mtaalamu wa mambo ya kishirikina ili amroge Kylian Mbappé huku Paul Pogba alikanusha vikali shutuma hizo.

Swala hili limeteka hisia za wengi sana kwenye mitandao. Inasemekana Kocha wa timu ya Taifa ya Ufaransa Didier Deschamps anafuatilia kwa ukaribu jambo hili ili ajue kile kinachoendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live