Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbappe abebeshwa zigo la Ronaldo

Mbappe X Hakimi Kylian Mbappe akmfariji Ashraf Hakimi

Thu, 15 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji wa Ufaransa na klabu ya Paris-Saint Germain, Kylien Mbappe amepandisha picha inayomuonyesha akiwa amekumbatiana na beki wa Morocco, Achraf Hakimi, lakini akajikuta anabebeshwa mzigo mkubwa na mashabiki; wamemtaka aifunge Argentina ili kumuenzi mshambuliaji wa Ureno, Christiano Ronaldo.

Jana usiku, Mbappe aliiongoza Ufaransa kuibwaga Morocco kwa mabao 2-0, bao la pili likiwa limetokana na ustadi wake wa kukatisha katikati ya mabeki wa Morocco na baadaye mpira kwenda kwa Kolo aliyesukumia wavuni akiwa hajazongwa. Katika fainali Jumapili, Ufaransa, ambao ni mabingwa watetezi, watakutana na Argentina ambayo iliitoa Croatia kwa mabao 3-0 katika mechi nyingine ya nusu fainali iliyoichezwa Jumanne.

Katika ukurasa wake wa Instagram wa @k.mbappe unaofuatiliwa na watu milioni 77.8, Mbappe ameweka pia picha inayomuonyesha akiwa amezungukwa na wachezaji wa Morocco katika tukio linaloonekana kuwa ndilo lililozaa bao la pili huku Hakimi akiwa anagaagaa chini.

“Back to back World Cup Final,” ameandika Mbappe chini ya picha hiyo akimaanisha anarejea fainali kwa mara ya pili mfululizo na kuweka emoji ya bendera ya Ufaransa.

Ameongeza kuandika “usihuzunike sana kaka, kila mtu anajivunia ulichofanya, umeandika historia”, maneno ambayo yanaonekana yanalenga kumfariji Hakimi ambaye kwa mara ya kwanza ngome yake iliruhusu wachezaji wa timu pinzani kutikisa nyavu za wababe hao wa Afrika Kaskazini katika fainali za mwaka huu za Kombe la Dunia.

“Nakupenda kaka,” amejibu Hakimi na kuungwa mkono na watu 114,374 walioweka alama ya “like” huku zaidi ya watu 700 wakimjibu kwa kuweka alama za moyo, bendera za Morocco na Ufaransa, moto, makofi ya kushukuru na msuli, kuonyesha kumuunga mkono.

Kati ya wafuasi 62,081 waliokuwa wametoa maoni yao hnadi leo saa 7:30 mchana, wapo waliokubaliana na kitendo chake cha kuposti picha hiyo wakimuona kuwa muungwana na wako waliombebebesha jukumu hilo la kuhakikisha anaiongoza Ufaransa kuishinda Argentina ili kumuenzi Ronaldo, ambaye hakuwa na fainali nzuri baada ya kuanzia benchi katika mechi mbili za hatua ya mtoano na Ureno kutolewa katika robo fainali.

“Shinda (Kombe la Dunia) kwa ajili ya CR7 na Hakimi,” ameandika mfuasi anayejiita diopratana95. “Ishinde Argentina kwa ajili ya Ufaransa, mshinde Messi kwa ajili ya Ronaldo,” ameandika mfuasi mwingine anayejiita grisha960w.

“Haki kwa Ronaldo, twende Ufaransa,” ameandika tinayen05, huku mwingine, nlkhjil-sharma015, akiandika “Ronaldo yuko ndani ya gari lake.. una uhakika na hilo… mashabiki ## wa plastilki wa Morocco wanaomchukia Ronaldo… hata baada ya kujua anatoa msaada kwa nchi yenu maskini. Nyinyi mnastahili kuona timu yenu ikishindwa… rudini na mpandishe ufahamu wenu wa soka na mjifunze kuheshimu maghwiji wakati nchi yenu haiwezi kuwa naye hata mmoja ### ombaomba”.

Mwingine amechukulia ushindi huo wa mabao 2-0 kuwa ni malipo ya kisasi kwa niaba ya Ronaldo. “Tunakushukuru kwa kumlipia kisasi Ronaldo, tunatumaini utashinda, tunakupenda,” ameandika erdem-kardas-official.

Mbali na kumtaka aiongoze Ufaransa kuishinda Argentina katika fainali Jumapili ili kumuenzo Ronaldo, wapo wafuasi ambao wamemponda na kumwambia hatafua dafu kwa Messi. Baadhi wametoa maoni yao kwa Kifaransa, wengine kwa Kiingereza, wengine Kireno na Kijerumani.

Chanzo: Mwanaspoti