Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbappe aachwa pre-season PSG

Mbappe Nahodha Mpya Ufaransa Amrithi Lloris Kylian Mbappe.

Sat, 22 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya PSG imemuacha mshambuliaji Kylian Mbappe nje ya kikosi cha klabu hiyo kilichoelekea Japan kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya (pre-season) baada ya Mfaransa huyo kugoma kusaini nyongeza ya mkataba mpya.

Mkataba wa Mbappé na vigogo hao wa Ufaransa utafikia ukomo msimu ujao huku klabu hiyo ikiwa haipo tayari kuruhusu nyota huyo kuondoka bila malipo mwisho wa mkataba wake msimu ujao.

PSG ilimpa Mbappe machaguo mawili ambayo ni aidha asaini nyongeza ya mkataba mpya au auzwe wakati wa dirisha hili la usajili. Kuachwa kwa Mbappé kunamaanisha PSG imekubali kumuuza nyota huyo sasa ili kuepuka kumruhusu kuondoka bila malipo msimu ujao.

Naye Mbappé ameendelea kusisitiza kuwa hayupo tayari kuondoka klabuni hapo licha ya vilabu kadhaa kummezea mate ikiwemo Real Madrid.

PSG imemuacha Mbappé nje ya mipango ya pre-season ikiwa ni katika jitihada za kutaka abadili msimamo wake wa kuamua kusaini nyongeza ya mkataba mpya au kuondoka klabuni hapo kwa malipo.

Ni nini kitafuata ikiwa Mbappé ataendelea kusimamia kusalia klabuni hapo ilihali PSG haipo tayari kumruhusu kuondoka bila malipo msimu ujao.?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: