Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbappe: Siondoki PSG ng'o

Mbappe Deja 1140x630 Mbappe: Siondoki PSG ng'o

Fri, 11 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kylian Mbappe ameiambia Paris Saint-Germain kwamba hataondoka msimu huu wa joto kwa hali yoyote, kulingana na ripoti.

Nahodha huyo wa Ufaransa bado yuko kwenye mvutano na klabu hiyo kutokana na kushindwa kuongeza mkataba na klabu hiyo ya Ligue 1.

Siku ya Jumanne PSG ilianza kuondoa bango kubwa la Mbappe kwenye uwanja wa Parc des Princes, baada ya kwanza kumhukumu kucheza na timu B ya klabu hiyo na kutomchagua kushiriki katika ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya barani Asia.

Jezi ya Mbappe pia imeondolewa kwenye duka la klabu, wakati uongozi wa Paris ukijaribu kumlazimisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kukubali mkataba wa kudumu au uhamisho wa mkopo ambao utaifanya klabu hiyo kurejesha pauni milioni 250.

Mbappe huwenda akafungiwa kabisa na PSG kutocheza hadi mwisho wa mkataba wake mwaka 2024, huku matajiri hao wa Ufaransa wakiamini nyota huyo anakusudia kuhamia Real Madrid kama mchezaji huru.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: