Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbappe: Ronaldo apewe heshima yake

Mbappe Ronaldo Mbappe: Ronaldo apewe heshima yake

Wed, 31 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

mshambuliaji wa Klabu ya PSG na Timu ya Taifa ya Ufaransa, Kylian Mbappe amesema kuwa vyombo vya habari vinapaswa kumpa heshima yake legendary wa soka duniani, Cristiano Ronaldo kutokana na mambo makubwa aliyofanya kwenye tasnia hiyo.

Mbappe amedai kuwa ni vyema vyombo vya habari vikanyamaza kama vinashindwa kumpa heshima inayostahili staa huyo wa Ureno.

"Alichofanya Cristiano Ronaldo akiwa na Juventus katika misimu mitatu kinachukuliwa poa sana, alienda akiwa na umri wa miaka 34 na kufunga mabao zaidi ya 100+ kwenye ligi yenye Mabeki wagumu zaidi Duniani.

"Wakati mwingine nadhani hawapimi kwa yote aliyofanya, vyombo vya habari heri vinyamaze kuliko kuendekea kumkosea," amesema Mbappe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live