Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbappe, Lewandowski wapinga Kombe la Dunia kufanyika baada ya miaka miwili

Mbappe Lwandowski Mbappe, Lewandowski wapinga utaratibu wa Kombe la Dunia kufanyika kila baada ya miaka miwili

Tue, 28 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa kati wa Ufaransa Kylian Mbappe na mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski kwa pamoja wamepinga utaratibu pendekezwa wa kufanyika kwa Kombe la Dunia kila baada ya miaka miwili.

Utaratibu huo pendekezwa umekuwa ukipigiwa chapuo na Shirikisho la Kabumbu Duniani Fifa kuwa Kombe la Dunia liwe linafanyika kila baada ya miaka miwili tofauti na sasa ya miaka minne.

Moja ya hoja ya Fifa ni kuwa Kombe la Dunia likifanyika kila miaka miwili kutakuwa na ongezeko la fedha kutoka kwenye makampuni kwa ajili ya Ustawi wa kandanda pamoja na kuwapa nafasi wachezaji kucheza michuano hiyo ya heshima mara nyingi.

“Kombe la Dunia, ni Kombe la Dunia tu, ni kitu maalumu”, alisema mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe.

“Kufanyika kila baada ya miaka miwili, ndiyo huongeza ushindani na ashiki ya kulifuatilia. Pia ameongeza kuwa “kufanyika kila baada ya miaka miwili itaongeza uchovu kwa wachezaji na kupoteza ubora wake”.

Jambo hilo limeungwa mkono na Robert Lewandowski nyota wa Bayern Munich mbaye amesema;

“Tuna mechi nyingi sana kwa mwaka, wiki ngumu baada ya ngumu, siyo tu michezo bali hata maandalizi ya mashindano makubwa”, alisema Lewandowski, 33.

“Kama unahitaji kuona kitu bora, tunahitaji mapumziko pia”, Aliongeza.

Shirikisho la Soka Afrika CAF linaunga mtindo huo wa Kombe la Dunia kufanyika mara mbili wakati lile la America Kusini Conmebol na Ulaya yakipinga utaratibu huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live