Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbappe, Kane ngoma droo UCL

Kylian Mbappe Bayern Munich Harry Kane Mbappe, Kane ngoma droo UCL

Wed, 6 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Washambuliaji Kylian Mbappe wa PSG na Harry Kane wa Bayern Munich wamelingana idadi ya mabao ya kufunga kwenye Ligi ya mabaingwa barani Ulaya (UCL) msimu huu 2023-24. Wote wana mabao 6, na timu zao zimefuzu hatua ya robo fainali.

Usiku wa jana Mbappe na kane wote walifunga mabao 2 kila mmoja na kufikisha mabao 6. Kane alifunga mabao 2 kwenye ushindi wa mabao 3-0 walioupata Bayern Munich dhidi ya Lazio kwenye mchezo wa mkondo wa pili wa 16 bora.

Mbappe nae alifunga mabao yote 2 ya ushindi ya PSG dhidi ya Real Sociedad mchezo ambao PSG iliibuka na ushindi wa mabao 2-1. Sasa mbappe na Kane ndio vinara wa mabao wakiwa na mabao 6.

Wachezaji wengine ambao bado wapo kwenye mashindano na wanaweza kuwafikia kane na Mbappe ni Álvaro Morata na Antoine Griezmann wote wa Atlético Madrid, Erling Haaland wa Man City, na Galeno wa FC Porto wote hawa wana mabao 5 na timu zoa zina michezo ya 16 bora.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live