Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbao yatakata Kirumba, yainyuka Nyaishozi 3-2

Mbao Fc 1 Timu ya Mbao FC

Fri, 29 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Timu ya Mbao imeibuka na ushindi wa mabao 3-2 nyumbani katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa wakiizaba Nyaishozi FC ya Karagwe mkoani Kagera katika mwendelezo wa Ligi Daraja la Kwanza (First Division League).

Mchezo huo umepigwa leo saa 10 jioni katika uwanja huo bila vinendera ambavyo vilichomekwa dakika tatu baadaye, huku Mbao wakiwa wa kwanza kuandika bao mnamo dakika ya pili kupitia kwa nahodha wake Ndaki Robert aliyewachambua walinzi na kufumua shuti lililozama moja kwa moja nyavuni.

Bao hilo la mapema liliwazindua Nyaishozi kutoka usingizini ambao walianza kusuka mipango ya kusawazisha na kufanikiwa mnamo dakika ya tano likifungwa na Credo Patrick na kuongea la pili katika dakika ya 14 likifungwa na Egon Rutandula.

Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika wageni Nyaishozi FC walienda kifua mbele wakiongoza kwa mabao 2-1.

Kipindi cha pili Mbao waliamka na kuja juu wakitaka kutafuta mabao ambapo jitihada zao zilizaa matunda mnamo dakika ya 61 likifungwa na Nasri Aziz na kuongea la tatu na la ushindi lililojazwa kimiani na Nasoro Iddi.

Nahodha wa Mbao, Ndaki Robert amewasihi mashabiki kuendelea kuiunga mkono timu hiyo iweze kufanya vyema na kurejea Championship, huku Kocha wa Nyaishozi, Moses Richard akisema kipigo hicho walistahili kwa sababu timu haina morali ikikabiliwa na ukata ambao unawapa mashaka ya kuendelea na ligi.

Hata hivyo, ilishuhidiwa Mbao ikiongozwa na Kocha Ibrahim Mulumba na Hassan Shehata huku aliyekuwa Kocha wa timu hiyo Athuman Cairo akibwaga manyanga baada ya kuiongoza kwenye mechi mbili za ligi hiyo.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz