Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbao FC, wababe wa Yanga na Simba wanaopumulia mashine

Mbao FcKL 1 Mbao FC, wababe wa Yanga na Simba wanaopumulia mashine

Fri, 24 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa klabu ya soka ya Mbao FC yenye maskani yake Ilemela jijini Mwanza ambayo imewahi kutamba ligi kuuTanzania bara kwa kuzifunga timu za Simba na Yanga Almas Mosh amesema kamwe timu yake haitashuka daraja kucheza ligi ya mkoa licha ya kutofanya vizuri kwenye mashindano ya First League ambayo yanaendelea hivi sasa kwenye maeneo balimbali hapa nchini.

Moshi amesema kuwa “ni kweli kwa msimu huu hatukufanya vizuri kwenye mashindano ya ligi daraja la pili (Firt League) hilo lilitokana na ushindani uliopo kwenye hayo mashindano pamoja na ukosefu wa fedha wa kukamilisha baadhi ya mipango ili timu iweze kucheza soka”

“Lakini kwa hali tuliyonayo kwa sasa tunapambana usiku na mchana kuhakikisha kwamba tunabaki ligi daraja la pili maarufu kama First League ili msimu ujao tujipange tena kuona kama tunaweza kupanda daraja kucheza Championship na mkakati huo tumeshauanza na tunaamini kwamba hatushuki kwenda kucheza ligi ya mkoa wa Mwanza”

Mbao FC ambayo inamilikiwa na aliyekuwa mkurugenzi wa ufundi wa TFF Amy Ninje iko nafasi ya nane kwenye msimamo wa kundi B wakiwa na jumla ya alama moja baada ya michezo nane, Mbao FC ni miongoni mwa timu ambazo ziliweza kutoa ushindani mkubwa kwa timu za Simba na Yanga kwenye uwanja wa CCM Kirumba lakini hivi sasa wako mahututi wakipumulia mashine wakipambana kujinasua na janga la kushuka daraja.

Mbao ili wabaki daraja wanatakiwa kushinda michezo sita iliyobaki katika kundi B ili wafikishe jumla ya alama 19 ambapo kama sio kushuka wanaweza kucheza Play off a kujinasua na janga la kushuka daraja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live