Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbangula sasa awavaa Aziz Ki, Fei vita ya ufungaji

Mbangula Prisonss Mbangula sasa awavaa Aziz Ki, Fei vita ya ufungaji

Sun, 10 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Straika wa Tanzania Prisons, Samson Mbangula amesema mabao mawili aliyofunga katika mechi iliyopita dhidi ya Simba yamempa matumaini ya kujiweka kwenye vita ya kuwania kiatu cha mfungaji bora Ligi Kuu.

Nyota huyo ambaye ameonekana kuwaka kwa sasa, tayari ametupia mabao saba na kuachwa matano dhidi ya kinara, Feisal Salum wa Azam aliye na 12 na Ki Aziz wa Yanga mwenye 11.

Mbangula amejiwekea rekodi tamu akimtibulia Kocha Mkuu wa Simba, Abdelakh Benchikha ambaye alikuwa hajaonja kisago kwenye Ligi Kuu, pia kuwa mchezaji aliyefunga katika michezo minne mfululizo.

Nyota huyo alisema licha ya kwamba ni mapema, lakini kwa kasi aliyoonyesha imempa matumaini lolote linaweza kutokea iwapo ataendelea kukaza kwa kila mechi kufunga bao.

“Kama nitaendelea kutumia nafasi ninazopata lolote linawezekana, nashukuru ushirikiano na wenzangu kikosini na kila mmoja anapambana kuipa matokeo timu.”

“Malengo yetu ni kuona tunashinda kila mechi ili kujua mwisho wa msimu tunaangukia nafasi ya ngapi, kimsingi mashabiki waendelee kutusapoti na tunahitaji hata nafasi nne za juu,” alisema askari huyo.

Juzi Jumamosi, Tanzania Prisons ilikuwa Uwanja wa Manungu Morogoro dhidi ya Mtibwa Sugar na kuambulia kichapo cha mabao 2-1.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: