Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbangula, Zabona waizamisha Tabora United

Prisons FC Mbangula, Zabona waizamisha Tabora United

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kolabo ya Zabona Hamis na Samson Mbangula wa Tanzania Prisons imeendelea kuzitesa timu pinzani baada ya jioni ya leo, Jumatano, kuizamisha Tabora United kwa mabao 2-1 katika pambano kali la Ligi Kuu Bara lililochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.

Wawili hao wamekuwa na maelewano mazuri uwanjani wakihusika katika ushindi wa mechi tano kati ya saba walizocheza Tanzania Prisons na kuiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi hiyo iliyopo raundi ya 18.

Katika mechi nane tangu atue Kocha Mkuu, Ahmad Ally akiziba nafasi ya Fred Felix 'Minziro' wameshinda mitano dhidi ya Dodoma Jiji 1-0, Mashujaa 2-0, Singida 3-1, Namungo 1-0 na leo dhidi ya Tabora United ilhali sare mbili ni mbele ya Ihefu na Azam na kupoteza mmoja kwa Yanga 2-1.

Wakicheza katika mwendelezo wa ubora wameikanda Tabora United na kutimiza ahadi ya kulipa kisasi dhidi ya wapinzani wao hao baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora kulala kwa mabao 3-1.

Katika mchezo wa leo Prisons ilipata mabao hayo kila kipindi, Zabona akianza katika dakika ya 21 likiwa ni la kusawazisha baada ya Eric Okutu kuwatanguliza wageni dakika ya 18 mabao yaliyodumu hadi mapumziko, ndipo Mbangula alipoongeza la pili na la ushindi dakika ya 85 na kuiwezesha timu hiyo kuzoa pointi tatu zikiifanya ifikishe alama 24 na kuchumpa nafasi ya tano.

Bao la Okutu limemfanya afikishe sita, huku Mbangula akifikisha matano na Zabona likiwa ni la nne katika mechi za msimu huu.

Tabora imefikisha mchezo wa nane mfululizo bila kupata ushindi ikiwa ni sare tatu dhidi ya Namungo 1-1, Mashujaa 1-1, suluhu mbele ya Azam na Singida United 1-1, huku ikipoteza mitano kwa Ihefu 2-1, Yanga 1-0, Simba 4-0 kabla ya leo kuloa tena.

Kwa Mbangula anaendeleza ubora wa kufunga mabao katika mechi tatu mfululizo akianza dhidi ya Singida Foutnatin Gate kisha Azam na leo anatupia tena, huku Zabona akifikisha mabao manne na asisti nne.

Matokeo hayo yanaifanya Tabora United iliyo chini ya kocha Goran Kopunovic aliyewahi kuiongoza Simba ikiendelea kusalia nafasi 13 kwa alama 18.

Chanzo: Mwanaspoti