Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbangula: Simba wamefanya makosa mwili

Mbangula Prisonss Samson Mbangula.

Thu, 7 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Klabu ya Soka ya Tanzania Prisons, Samson Mbangula amesaema kuwa licha ya kuwafunga SImba SC, bado timu hiyo ni bora na hawezi kuidharau kwani imekuwa na ikifanya vizuri kwenye Ligi ya ndani na Klabu Bingwa Afrika.

Mbangula amesema hayo baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Simba uliopigwa jana Februari 7, 2024 katika Dimba la CCM Jamhuri Morogoro huku akifunga mabao yote mawili na kuipa timu yake ushindi wa bao 2-1.

“Tanzania Prisons tunapambana tupate matokeo, sio kwa mechi hii tu, mechi nyingi tumekuwa na mwendelezo wa kufanya vizuri na kupata matokeo. Hata leo tulikuwa kwenye kiwango bora, ukiacha mimi bali timu nzima imecheza vizuri. Mimi si kitu mbele ya wenzangu, wao ndiyo wanafanya kazi kubwa ya kunitengenezea nafasi na nikafunga mabao mawili.

“Siwezi kusema Simba ni wabovu, ukisikia mpira ni mchezo wa makosa ndiyo hivyo, ukifanya kosa unaadhibiwa na mpinzani, hii inatokea kwenye soka. Simba wamefanya makosa mawili tu kwenye mechi nzima na ndiyo hayo tumeyatumia kuwaadhibu.

“Malengo ya mchezaji ni kufanya kile anachonuia moyoni mwake, namshukuru Mungu naendelea kufunga na leo ni bao la saba, tunaendelea kupambana. Nina malengo ya kufikisha bao kadhaa ila siwezi kusema ngapi. Kuhusu mbio za ufungaji bora ni mapema sana kuzungumzia kwa sasa.

“Simba ni timu bora siwezi kuwadharau kwa sababu heti tumewafunga. Mechi iliyopita ya CAFCL dhidi ya Jwaneng walicheza vizuri walikuwa na kiwango bora. Kwenye soka inatokea, unafanya makosa unaadhibiwa.

“Msimu uliopita hatukuwa na mwendelezo mzuri sana mpaka tukanusurika kushuka daraja, mwalimu ameliona hilo ndiyo maana akaja na mpango kazi mzuri ambao tunautekeleza ili yasijirudie ya mwaka jana na tuwe kwenye nafasi nzuri.

“Hakukuwa na sapraizi kubwa kihivyo, sisi tulikuwa na game plan, mwalimu akaja na game plan yake tuliipokea vizuri na kuutekeleza. Imetokea wenzangu wametengeneza nafasi mimi nikafunga basi, ndivyo game ilivyokuwa,” amesema Mbangula.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live