Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbangula Shujaa wa Prisons aliyeizamisha Simba

Mbangula+pic Mbangula Shujaa wa Prisons aliyeizamisha Simba

Sat, 24 Oct 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By YOHANA CHALLE MASHABIKI wa Simba hawana hamu hata kidogo na Tanzania Prisons. Ni timu ambayo kwa misimu kadhaa imekuwa ikiwasumbua na juzi kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara msimu huu, iliwaliza kwa kuwatungua bao 1-0.

Bao hilo pekee la dakika ya 49 lilitibua rekodi waliyokuwa nayo ya kucheza mechi 10 mfululizo za mashindano kwa muda wa siku 98 ambazo ni sawa na saa 2, 352 bila kuonja kipigo chochote.

Zile kelele la Simba pira biriani...pira pishori na kelele nyingine za mashabiki wa Simba zilizimwa na pira gwaride kupitia mpira wa kichwa uliopigwa kiufundi na mshambuliaji Samson Mbangula mbele ya beki kisiki, Joash Onyango na kumuachia msala kipa Aishi Manula.

Kwenye mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga mkoani Rukwa, Simba ilionekana kupoteza soka lake tamu, pengine kutokana na kukosekana kwa nyota wake kadhaa ikiwamo injini yao, Clatous Chama na mitambo ya mabao - Meddie Kagere, John Bocco na Chris Mugalu.

Alichokifanya Mbangula kimeipa jeuri Prisons kumaliza ukame wa misimu minne bila kushinda mbele ya Wekundu wa Msimbazi. Mara ya mwisho Prisons kuifunga Simba ilikuwa msimu wa 2016-2007 walipoifumua nyumbani mabao 2-1 kipindi hicho ikicheza jijini Mbeya.

MSIKIE MBANGULA

Chanzo: mwanaspoti.co.tz