Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbadala wa Morrison atua Dar, Yanga kazi kwao

Maxi Nzengeli Gd Nahodha wa AS Maniema Union ya DR Congo, Maxi Mpia awasili Dar

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa AS Maniema Union ya DR Congo, Maxi Mpia amewasili nchini mchana wa leo Julai 12, 2023 kukamilisha dili la kujiunga na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga.

Maxi kama mambo yataenda sawa msimu ujao atavaa uzi wa njano na kijani ambapo taarifa za kupenyezewa zinadai Yanga watalazimika kutumia zaidi ya Sh400 milioni kununua mkataba wake wa mwaka mmoja uliobakia kwenye klabu yake ya AS Maniema.

Winga huyo anatajwa kuja kuchukua nafasi ya Mkongomani mwenzake Twisila Kisinda aliyeimaliza mkataba wake wa mwaka wa mkopo akitokea RS Berkane ya Morocco.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: