Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbabe wa Yanga kuumana na mbabe wa Afrika leo

Mbabe Wa Yanga Kuumana Na Mbabe Wa Afrika Leo.jpeg Mbabe wa Yanga kuumana na mbabe wa Afrika leo

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbabe wa Yanga SC, CR Belouizdad leo naye atakuwa dimbani kuchuana na mbabe wa Afrika, Al Ahly.

Al Ahly leo atakuwa nyumbani kumualika Belouizdad aliyetofautiana naye alama moja tu kwenye msimamo wa kundi lao, Kundi D.

CR alimfunga Yanga 3-0 kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza kisha naye akafungwa na Medeama 2-1 katika mechi ya mzunguko wa pili.

Msimamo wa kundi lao, Al Ahly anaongoza akiwa na alama 4 akifuatiwa na CR mwenye alama 3 kisha Medeama ambaye naye ana alama 3 huku Yanga akiburuza mkia akiwa na alama 1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live