Klabu ya Wydad Casablanca ya nchini Morocco, huenda ikatangaza kuachana na mshambiliaji wa kimataifa kutoka Senegali, Bouly Sambou (24), kwa kile kinachodaiwa kuwa mchezaji huyo tayari amepata timu nyingine kwaiyo anahitaji kuondoka.
Taarifa kutoka nchini Misri zinaarifu kuwa Sambou hajawasili mazoezini kwenye club ya wydad Casablanca.
Sambou bado amebakisha mkataba wa miaka mitatu kwenye kwa mkataba wake ambao unatamatika June 2026, na nyongeza ya mkataba.
Sambou ndiye aliefunga goli la kusawazisha dhidi ya Simba SC Kwenye uwanja wa Mohamed Wa V Katika hatua ya Robo Fainali msimu jana. Hata hivyo Simba waliondolewa kwa changamoto ya mikwaju ya Penati.