Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mbabe wa Azam arejea Yanga, kazi ipo Jumapili

Musonda Farid M Mbabe wa Azam arejea Yanga, kazi ipo Jumapili

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Yanga raia wa Zambia, Kennedy Musonda amerejea kikosini akiwa imara baada ya kupona majeraha.

Musonda alianza vyema msimu kabla ya kupata majeraha ambayo yamemfanya aingie na kutoka kikosini kwa nyakati tofauti.

Yanga imethibitisha kuwa Musonda amepona kwa asilimia 100, Farid Mussa akiwa mchezaji pekee ambaye anaendelea kuimarika kutoka kwenye majeraha.

Unaweza kusema mshambuliaji huyo kutoka Zambia bado ana deni kubwa kutoka Wananchi kwani baada ya kuondoka Fiston Mayele, wengi walitarajia yeye kuwa ndiye mshambuliaji kiongozi.

Badala yake kocha mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amekuwa akimtumia kinda Clement Mzize zaidi Musonda akikosekana baadhi ya mechi akiwa majeruhi.

Jumapili ya wiki hii Yanga itashuka uwanja wa Azam Complex kumenyana na Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC

Musonda ana kumbukumbu nzuri mbele ya Azam Fc, msimu uliopita alifunga bao pekee la ushindi katika mchezo wa fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) mchezo ukipigwa uwanja wa Mkwakwani.

Pengine hii ni mechi ambayo Musonda anaweza kuitumia kurejesha kasi yake ya kuzifumania nyavu. Katika msimu huu Musonda amefunga bao moja tu kwenye ligi kuu ya NBC.

Kwa upande wa Farid pia ana kumbukumbu nzuri dhidi ya waajiri wake wa zamani, Azam FC ambapo kwenye mchezo wa raundi ya pili msimu uliopita 2022/23, Farid alipigilia msumari wa ushindi na kuifanya Yanga kuibuka na ushindi wa bao 3-2.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live