KIKOSI cha Simba kinaendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa Ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita ambao utachezwa Aprili 3, katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Kocha wa Simba, Adel Zrane anasema kikosi chao tangu kuanza kwa wiki hii wamekuwa wakifanya aina ya mazoezi mbalimbali ya nguvu na mbinu.
Gomes anasema kuna siku ambazo wanafanya mazoezi kwa awmu mbili (Gym), pamoja na uwanjani yakilenga nguvu na pamoja na mbinu ili kuwaweka katika hali ya utimamu wa mwili kama wale ambao wapo katika timu zao za taifa.
Amesema maandalizi haya ni kwa ajili ya mechi yao ya Ligi ya mabingwa Afrika ambayo watacheza siku chache baada ya wachezaji wote kurejea na kuungana kwa pamoja.
"Baada ya wachezaji kukutana kwa pamoja kutoka katika majukumu ya timu zao za taifa tutakuwa na muda mfupi kabla ya kucheza na AS Vita ndio maana tuliobaki nao tunafanya nao maandalizi ya kutosha," amesema Gomes.