Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mazembe watia dosari sherehe za Simba Day

E QuVf9X0AQ0nEF Mtanange wa Simba vs TP Mazembe

Mon, 20 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya TP Mazembe na mabingwa mara tano wa kombe la Afrika, wameonesha ukubwa wao baada ya kuwatandika mabingwa mara nne mfululizo wa Tanzania, Simba Sports Club katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.

Simba wakiwa na sapoti ya Mashabiki waliofurika katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam wameshindwa kufanya lolote kutoka kwa wababe hao kutoka DR Congo na kukubali kichapo cha bao 1-0.

Bao la TP Mazembe limewekwa kimiani na Jean Beleke 84' baada ya makosa ya mlinda mlango wa Simba na limedumu mpaka zinakamilika dakika 90.

Hii ni mechi ya kwanza kwa mashabiki wa Simba kuona timu yao ikicheza na kuhudhuriwa na mashabiki wake tangu walipoanza maandalizi ya kujiandaa na msimu mpya 2021/2022.

Katika mechi hiyo dhidi ya Mazembe Simba ilipata nafasi ya kuwachezesha nyota wake wengi waliosajiliwa dirisha lililopita, wakiwemo Kibu Denis,Duncan Nyoni,Konate,Sakho.

Simba itakutana na Yanga Septemba 25 katika mchezo wa Ngao ya Jamii kama sehemu ya ufunguzi wa Ligi kuu Tanzania Bara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live