Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mazembe 'kudesa' kwa Yanga kuna la kujifunza

Mazembez UAAmtP1.jpeg Mazembe 'kudesa' kwa Yanga kuna la kujifunza

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msafara wa Viongozi wa TP Mazembe ukiongozwa na CEO wao, Frederic Kitengie, wamefika Makao Makuu ya Klabu ya Yanga na kupokelewa na Mtendaji Mkuu wetu, Andre Mtine kwaajili ya ziara rasmi.

Klabu ya Yanga kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii wametaja ziara hiyo kuwa na dhima kuu ya TP MAZEMBE kujifunza kwa Yanga.

Klabu ya TP Mazembe ameshinda makombe yote ya ngazi ya klabu hapa Afrika , Yanga ndio kwanza tunaitafuta Fainali ya CAF Champions League, lakini TP Mazembe wamekuja kuchukua uzoefu kwetu Tanzania.

Mazembe wanavikumbusha vilabu vya Tanzania kuwa Elimu Haina mwisho, unaweza kujifunza hata kwa uliye mzidi na unaweza kufundisha ulio wazidi pia.

Njooni Jangwaani mjifunze

MAFANIKIO YA TP MAZEMBE MAKOMBE - Klabu Bingwa Afrika (×5) - Shirikisho (×2) - CAF super cup (×3) - Kombe la Washindi (×1) - Uwanja wao binafsi - 2023 /2024 CL (Nusu Fainali)

“Ni heshima kubwa kwetu na tumefurahi kwa mapokezi mazuri mliyotupatia, tumekuja hapa kujifunza kuhusu Yanga na kutengeneza urafiki mzuri utakaoweza kuvisaidia vilabu vyetu hivi viwili bora Afrika Mashariki na kati hivi sasa," amesema Frederic Kitengie - CEO TP Mazembe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live