Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele sasa anakitaka kiatu

Captureeeeee Mayele sasa anakitaka kiatu

Mon, 4 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji nyota wa Green Warriors, Kassim Shaibu ‘Mayele’ amesema moja ya malengo yake aliyojiwekea msimu huu katika Ligi ya Championship ni kumaliza kinara wa ufungaji bora, licha ya kukiri sio rahisi pia kutokana na ushindani mkubwa uliopo.

Akizungumza na Mwanaspoti jijini Dar es Salaam, Mayele alisema anafurahia kiwango alichonacho msimu huu, ingawa bado ana tamani kuendelea kufanya vizuri huku akiwamwagia sifa washindani wake kwa sababu ndio wanaompa changamoto ya kupambana.

“Vita ya ufungaji imekuwa kubwa sana kwa sababu kila mmoja anaonyesha uwezo alionao, hali hii inaongeza ladha halisi ya ushindani, nami nimejipanga kukabiliana nayo katika mazingira ya aina yoyote ili nifikie malengo kwa msimu huu,” alisema.

Akizungumzia chimbuko la jina hilo la Mayele, alisema alipewa wakati akiichezea timu ya Lumo Combine ya Buza jijini Dar es Salaam wakati wa ‘Ndondo Cup’ kutokana na upambanaji wake akifananishwa na nyota wa zamani wa Yanga Mkongomani, Fiston Mayele.

Nyota huyo aliyejiunga na timu hiyo msimu huu baada ya kuondoka Mbeya Kwanza, hadi sasa tayari amefunga mabao saba akiwa na kikosi hicho akipitwa na Edgar William wa KenGold mwenye 10 na Ramadhan Kapera wa Mbeya Kwanza aliyefunga tisa.

Chanzo: Mwanaspoti