Jumamosi iliyopita kulishuhudiwa mchezo wa hisani wa kuchangia vifaa vya Mama wajawazito ulioadhaminiwa na Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) kwa kuzikutanisha timu Feitoto dhidi ya timu Bui, ambapo mastaa kibao wa soka kutoka ndani na nje ya mipaka ya Tanzania walishiriki.
Mchambuzi Kheir Salum wa Asubuhi Njema ya ZBC anasema, mashabiki waliofika uwanjani kwenye mchezo huo walionyesha mapenzi yao kwa mshambuliaji wa Yanga SC, Fiston Mayele jambo lililopelekea itumike nguvu ya ziada na muda mrefu kumtoa nyota huyo uwanja kuelekea kwenye gari ya nje uwanja.
Mayele ambaye naye alionyeshwa kushangazwa na mapenzi hayo mazito ya Wazanzibar, amempongeza Feisal kwa mchezo huo wa kuwasaidia Mama wajawazito na kuahidi kuwa ni lazima atarejea tena Zanzibar.
Mayele ndiye Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara, pia ndiye mchezaji Bora wa Msimu na mshindi wa tuzo ya bao bora la msimu.