Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele mechi 13, mabao 3

Mayele MsA Mayele mechi 13, mabao 3

Tue, 16 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Pyramids FC ya Misri, Fiston Kalala Mayele amekuwa na wakati mgumu ndani ya kikosi hicho baa ya kushindwa kufanya vizuri.

Mayele amefanikiwa kucheza mechi 13, amefunga mabao manne pekee na pasi mbili za mwisho (assists).

Mayele jana alifanikiwa kufunga bao lake la nne ndani ya Ligi Kuu ya Misri katika ushindi wa bao 2-0 ambao Pyramids waliupata ugenini shidi ya Al Arab huku bao jingine la Pyramids likifungwa na El Karti dakika ya 8.

FT: PL AL ARAB 0-2 PYRAMIDS FC ⚽️ 8” El Karti ⚽️ 73” Mayele.

Mayele ambaye amewahi kuitumikia Yanga, alifanikiwa kuteka nyoyo za mashabiki wa timu hiyo akifunga mabao zaidi ya 50 kwenye michuano yote na kuyibuka kinara wa ufungaji bora msimu wa 2022/23 akifunga mabao 17.

Mayele aliibuka kinara pia wa mabao kwenye michuano ya CAFCC msimu huo akifunga mabao 7 na kuingia kwenye kinyang'anyiro cha wachezaji bora Afrika kwa msimu huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live