Katika vikosi vya sasa vya Yanga na Simba, Fiston Mayele ndie kinara wa kutupia kwenye mechi za dabi akiwa ametupia mabao matatu katika mechi 5 alizocheza dhidi ya Simba tangu ajiunge na Yanga
Katika mchezo wa Ngao ya Jamii uliopigwa kabla ya msimu kuanza, Mayele alikaribia kufikia rekodi ya mzee Abdallah Kibadeni ambaye ndie mchezaji aliyewahi kufunga Hat-trik katika mechi za Dabi
Mayele alifunga mabao yote mawili katika ushindi wa 2-1 ambao Yanga waliupata dhidi ya Simba na kutetea Ngao ya Jamii kwasimu wa pili mfululizo
Jumapili ijayo Oktoba 23 Mayele atakiongoza kikosi cha Yanga katika mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Simba msimu huu
Mcongomani huyo amekuwa na mwanzo mzuri msimu huu akipachika mabao 12 katika mechi 10. Mabao 2 Ngao ya Jamii, mabao matatu kwenye ligi na mabao 7 ligi ya bingwa Afrika.
Mambo huko hayatulii wakiwaza namna ya kumkaba mtaalamu huyu wa kuchela na nyavu Wananchi wakiitaka heshima kwa kuendeleza utawala wao kwenye soka la Tanzania.