Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele kuandika rekodi mpya kwa Ihefu leo?

Mayele Congo Msk Fiston Mayele

Mon, 16 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Yanga ikijipanga kuikaribisha Ihefu leo Januari 16 mchezo wa Ligi Kuu NBC, Fahamu rekodi hizi za kinara wa upachikaji mabao wa Yanga, Fiston Kalala Mayele.

Fiston Mayele amefunga mabao 9 katika mechi 9 za nyumbani msimu huu katika NBC Premier league, mengi zaidi ya mchezaji mwengine yoyote.

Fiston Mayele katika mabao 14 aliyoyafunga kwenye NBC Primia Ligi msimu huu, mabao 10 ameyafunga kwa mguu wa kulia, mengi zaidi ya mchezaji mwengine yoyote.

Fiston Mayele katika NBC Premier Ligi msimu huu hadi sasa.

michezo 17

dakika alizocheza 1362

mabao 14

pasi za mabao 2

amehusika katika mabao 16

Ana wastani wa kuhusika katika bao kila baada ya dakika 85

mabao 10 (mguu wa kulia)

mabao 2 (mguu wa kushoto)

mabao 9 (nyumbani)

mabao 5 (ugenini)

atakuwa kibaruani dhidi ya Ihefu leo, na Ihefu ni miongoni mwa timu nne pekee ambazo hajawahi kuzifunga katika ligi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live