Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele hana bahati na kipa huyu!

Fiston Kalala Mayele Life Fiston Mayele

Sat, 17 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Fiston Mayele yupo kwenye kambi ya timu ya taifa ya DR Congo akijiandaa na mechi ya kuwania fainali za Kombe la Afrika (Afcon 2023) zitakazofanyika mwakani huko Ivory Coast, huku akiwa na tuzo mbili za Mfungaji na Mchezaji Bora wa msimu wa 2022-2023 wa Ligi Kuu Bara.

Kipa huyo ni Isihaka Hakimu wa Ruvu Shootinga ambaye kama ilivyo kwa makipa wengine walioidakia timu hiyo tangu msimu uliopita hadi msimu huu, walimnyima nafasi Mayele kuingia kwenye rekodi ya kuzitungua timu zote alizokutana nazo. Ruvu Shooting imeshuka daraja.

Isihaka ndiye kipa pekee ambaye hajatunguliwa na Mayele alipovaana naye kama ilivyokuwa kwa makipa wengine aliokutana nao kwenye ligi au michuano mingine ya ndani, akiwa amesajiliwa kupitia dirisha dogo na kumbania straika huyo timu hizo zilipokutana kwenye mechi ya ligi msimu huu.

Mayele hajaifunga Ruvu iliyoshuka daraja pekee baada ya Tanzania Prisons kukubali kutibuliwa, wikiendi iliyopita wakati Yanga ikishinda 2-0 kwenye Uwanja wa Sokoine, huku Simba ikifungwa mara mbili na mchezaji huyo kwenye Ngao ya Jamii, licha ya kuishindwa ndani ya Ligi Kuu Bara.

Isihaka alianza kama kipa namba tatu, kisha kupanda hadi kuwa kipa namba moja na alizungumzia rekodi hiyo ya kutotunguliwa na Mayele kama ilivyokuwa kwa makipa wengine walioidakia Ruvu tangu msimu uliopita alisema anajisikia fahari kutokana na ukweli straika huyo ana balaa uwanjani.

Kipa huyo alisema licha ya Mayele kuwa tishio, lakini alipokutana naye hakumuogopa bali aliongeza umakini ili asitunguliwe na kutibua rekodi ya Ruvu kwa mchezaji huyo misimu miwili mfululizo.

Alisema kma kipa alikuwa ni miongoni mwa wachezaji aliekuwa akimfuatilaia na kuangalia namna yake ya ufungaji na uchezaji jinsi ilivyo kwani sikutaka kufungwa naye.

“Kila kipa mzuri ni lazima ajichunge na mtu kama Mayele, kwani ni mshambuliaji asiyetabirika ndio maana nilikuwa najifungia kumsoma na kwa bahati tulipokutana naye sikuruhusu bao,” alisema Isihaka aliyedaka mechi ya Januari 23 na Yanga kushinda 1-0 kwa bao la kujifunga la beki wa Ruvu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: