Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele awatikisa mastaa Ulaya

Mayele Mtwara Mayele awatikisa mastaa Ulaya

Wed, 4 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Kalala Mayele amewatikisa baadhi ya wachezaji wa DR Congo ambao wanakipiga katika ligi mbalimbali barani Ulaya mara baada ya kufanikiwa kuwa mchezaji bora wa mwaka 2022 nchini humo.

Baadhi ya wachezaji waliokuwa wanawania tuzo hiyo sambamba na Mayele ni pamoja na Jackson Muleka anayekipiga Besiktas ya Uturuki, Duemerci Mbokani anayecheza Sportkring Beveren ya Ubelgiji, Chancel Mbemba wa Olympic Marseille ya Ufaransa na Yoane Wissa wa Brentford ya England.

Ukiachana na Mayele ambaye ameshinda tuzo hiyo ya mchezaji bora wa mwaka wa nchini humo, Yanga sasa inakuwa imefikisha jumla ya wachezaji wanne ambao wameshinda tuzo ya mchezaji wa mwaka yaani MVP.

Yannick Bangala alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu uliopita jambo ambalo lilimfanya pia staa huyo kushinda pia tuzo ya kiungo bora wa msimu.

Khalid Aucho yeye pia alifanikiwa kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Uganda kwa msimu uliopita.

Mchezaji wa mwisho kwa Yanga ni Stephane Azizi Ki ambaye yeye amefanikiwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu nchini Ivory Coast msimu uliopita kabla ya kujiunga na Yanga msimu huu.

Hivyo Yanga wanakuwa na wachezaji Mayele, Bangala, Aucho na Azizi Ki ambao wote ni wachezaji bora kwenye nchi nne tofauti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live