Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele awafuata Aziz Ki, Pacome na Guede

Traore Zambro Zc Mayele awafuata Aziz Ki, Pacome na Guede

Thu, 2 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Pyramids FC ya Misri, Mkongomani Fiston Kalala Mayele amebadilisha wakala kwa sasa atakuwa anasimamiwa na Zambro Management chini ya Zambro Traore.

Mayele amecheza Yanga kwa misimu miwili mfululizo akitokea AS Vita Club ya nyumbani kwao Congo na kuonesha kiwango bora sana huku akijizolea umaarufu hasa kwa staili yake ya kushangilia kwa kutetema, na sasa anasakata kabumbu huko Misri.

Wakati Pyramids wanamtaka Fiston Mayele walimpa kazi Zambro Traore japo alikuwa hana mawasiliano na Fiston Mayele ila baadae akaipata namba ya Mayele ambae nae Mayele akampa Zambro namba ya Jasmine ambae ni msimamizi wake, baadae dili likakamilika hata siku ya kusaini na kupiga picha za utambulisho mwamba alisimamia ipasavyo na sasa Mayele yupo zake Pyramids.

Zambro Traore amekuwa akitumiwa na vilabu vikubwa barani Afrika kukamilisha usajili wa wachezaji wanaowahitaji ndio maana amehusika kwenye dili la Fiston Mayele japo si mchezaji wake.

Ismaily, Zamalek, Pyramids mara zote huwa zinamtumia kwa wale wachezaji wanaowahitaji ambao klabu imeshindwa kuwafikia.

Zambro Traore yupo Bongo kwasasa kwenye mazungumzo juu ya mkataba mpya wa Stephen Aziz Ki ambae ni moja ya wachezaje wake wakiwemo Pacome Zouzoua, Yao Koussi pamoja na Joseph Guede aliejiunga na Yanga dirisha dogo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live