Straika hatari wa Yanga raia wa DR Congo, Fiston Mayele, ameibuka na kusema kuwa, amesikia kauli za viongozi wa Rivers United za kutaka kupindua matokeo, na kusema kwamba: “Wao waje tu tumalizane kwa Mkapa.”
Jumapili ya wiki hii, Yanga itawakaribisha Rivers United kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya mchezo wa marudiano war obo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kupata ushindi ugenini wa mabao 0-2.
Akizungumza nasi, Mayele aliweka wazi kuwa, yupo tayari kwa mchezo wa marudiano na Rivers na nia yao kubwa ni kufuzu hatua inayofuata ya Nusu Fainali.
“Tangu tulipopangwa na Rivers tulitamani sana kulipa kisasi jambo ambalo tunaamini litatimia kwa kuwa tayari tumeshawafunga kwao, kilichobaki kwa sasa waje kwa Mkapa tumalizane tu,” alisema Mayele.