Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele atua daraja la kwanza

Mayele Kassim Mayele Kasim.

Wed, 6 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfungaji bora wa michuano ya Ndondo Cup 2023 Mayele Kasim, amefanikiwa kupata timu ya Ligi Daraja la Kwanza baada ya kuonyesha uwezo mkubwa akiwa na timu yake ya Madenge FC ambao walifanikiwa kutwaa ndoo ya Ndondo Cup kwa mara ya pili mfululizo.

Madenge FC walifanikiwa kutwaa ndogo hiyo kwa kuifunga Kibangu Rangers, Jumapili iliyopita katika Dimba la Kinesi.

"Namshukuru Mungu kwanza nimekuwa mfungaji bora wa haya mashindano nikiwa nimefunga goli 5 kwangu mimi ni furaha kubwa sana.

Ni msimu wangu wa pili kwenye michuano ya Ndondo cup nilianza kushiriki msimu ulipoita na mwaka huu nimepata fursa hiyo tena, kwangu mimi Ndondo Cup ni sehemu ya kupata ajira na mwanzo wa safari nyingine.

"Mfano mimi nimepata timu inayoshiriki championship lakini nimetoka kwenye Ndondo Cup, nawaomba vijana Ndondo cup wachukulie kama sehemu ya kuanza kutimiza ndoto zao," amesema Mayele Kasim.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live