Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele atoa gundu CAF, atupia bao mbili

Mayele Goli 2.jpeg Fiston Mayele

Sat, 2 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa zamani wa Yanga anayekipiga kwa sasa Pyramids ya Misri, Fiston Mayele jioni hii amefunga mabao mawili yakiwa ni ya kwanza kwake katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wakati timu anayoichezea ilipolazimishwa sare ya 2-2 nyumbani na Nouadhibou ya Mauritania.

Katika mechi hiyo ya kukamilisha hesabu za Kundi A, huku timu zote zikishindwa kupenya robo fainali ikiziachia Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini iliyoongoza kundi kwa pointi 13 na TP Mazembe iliyomaliza na 10, Mayele alifunga mabao hayo yaliyokuwa ya kusawazisha akichomoa moja baada ya jingine la wageni waliotangulia kabla yao.

Wageni walianza kufunga bao dakika yua 64 kupitia kwa Bessam Ahmed, kabla ya Mayele kuchomoa dakika ya 73 na muda mchache baadae Nouadhibou iliongeza la pili dakika ya 82 kupitia Issa M'Bareck.

Wakati wageni wakiamini wanashinda mchezo huo Mayele alichomoa bao hilo dakika za majeruhi akimalizia pasi la Mohamed Chibi na kumfanya amalize mechi hizo za makundi akiwa na mabao mawili na asisti moja na kumaliza utata alioibua hivi karibuni dhidi ya mashabiki wa klabu ya Yanga akidai amefanyiwa ushirikina asifunge.

Mayele aliyeanzishwa katika kikosi cha kwanza kama ilivyokuwa katika mechi iliyopita ya ugenini dhidi ya Mazembe na kumalizika kwa suluhu alipotumika kwa dakika 82, kwenye mechi ya leo alitumika kwa dakika zote 90, lakini licha ya kufunga mabao hayo hayaisaidia timu hiyo kutoka mkiani mwa kundi hilo.

Chama hilo la nyota na mfungaji bora huyo wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita akiwa na Yanga, imemaliza mkiani ikiwa na pointi tano sawa na wapinzani wao ambao wamenufaika na matokeo ya junmla baina yao kwani katika mechi ya kwanza ilifungwa mabao 2-0 ugenini.

Mamelodi iliyoshinda bao 1-0 mbele ya TP Mazembe imemaliza kama kina wa kundi hilo la A ikifikisha pointi 13, zikiwa ni tatu zaidi ya zile za Wakongoman hao waliomaliza nafasi ya pili.

Mamelodi inakuwa ni moja ya timu tatu, ikiwamo Asec Mimosas ya Ivory Coast inayoweza kukutana na Yanga au Simba kama itashinda mbele la Jwaneng Galaxy ya Botswana kwenye mechi za hatua ya robo fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live