Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele atajwa kuwania Tuzo ya CAF

Mayele Bonge Mayele atajwa kuwania Tuzo ya CAF

Mon, 3 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Fiston Mayele amewekwa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Septemba wa Afrika.

Mayele amewekwa kupitia jarida la Habari za michezo la foot.afrika akiwa sambamba na nyota kadhaa wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya.

Mchakato wa kumpata mchezaji bora wa mwezi Septemba kwa mujibu wa jarida hilo ni kupitia njia ya kupiga kura katika tovuti ya www.foot.afrika ambapo mchezaji atakayepata kura nyingi ndiye atakayeibuka mshindi.

Miongoni mwa nyota waliotyajwa kuwania tuzo hiyo ni;

1. Fiston Mayele (Yanga SC na DR Congo) 2. Seko Fofana (RC Lens na Ivory Coast) 3. Boulaye Dia (Salernitana na Senegal) 4. Dango Ouattara (Lorient na Burkina Faso) 5. Karl Toko-Ekambi (Olympique Lyon na Cameroon)

Vigezo vya nyota hao kuchaguliwa kuwania tuzo hiyo ni kutokana na viwango vyao kuwa bora katika Ligi zao pamoja na mashindano ya kimataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live