Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele atafunga sana, atasumbua mabeki kwa sababu hizi

Mayele Goal Fiston Mayele, akishangilia mbele ya Mashabiki wa Yanga

Wed, 20 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati wa dirisha la Usajili Yanga walichokifanya ni kusajili atu katika eneo la Ushambuliaji, wakaleta watu wawili Heritier Makambo na Fiston Mayele.

Mshambuliaji anayeanza hivi sasa ni Mayele, kwenye mechi yake ya Kwanza dhidi ya Hasimu wa Yanga, Simba SC alifunga bao la ushindi, ni haki kusema hakuna beki anayetamani kukabana na mshambuliaji aina ya Mayele.

Mayele hutumika kama Mshambuliaji kiongozi kwenye mfumo wa 4:2:3:1 ambapo anatakiwa awepo kwenye "zone" ya 14 na 17 kama "Target man" wanaposhambulia na zone ya 11 ambapo mabeki wa kati wanaomkaba huwepo wakati wanaposhambuliwa.

Ila uchezaji wa Straika huyo umekuwa tofauti kabisa na matarajio ya mabeki wa upinzani.

Mayele hucheza kama namba 9 ya uwongo, yaani "false namba 9" kwa kulikimbia sana eneo analotakiwa awepo kwa kushuka chini na kutanua uwanja hivyo kutengeza "gap" kati yake na mabeki na kusababisha ugumu kwenye kumkaba.

Ushukaji chini huo na utanuaji uwanja kwenye "Half Spaces" umekuwa ukiwaogopesha mabeki kumfuata kwa kuhofu kutelekeza malindo yao ya ulinzi wanayopaswa kuyalinda hivyo kumuacha akiwa huru.

Uhuru anaopata Mayele baada ya kuwakimbia mabeki ndiyo huumiza wapinzani kwani huongeza idadi ya viungo katikati na kuipa Yanga faida ya kuwa na "Numerical Advantage" inayopelekea Yanga kupata chaguzi nyingi za pasi.

Kwa aina hii ya uchezaji wa Mayele usitegemee afunge magoli mengi kama mshambuliaji bali hutengeza njia za timu kupata magoli kupitia viungo washambuliaji.

Fiston Mayele anaweza kufanya yote haya kwa ufanisi wa juu kutokana na u-fiti wa utimamu wa mwili alionao, spidi ya juu kwenye ukimbiaji, kupenda na kui-enjoy kukimbia muda wote pamoja na akili kubwa ya kufikiria na ku-react haraka bila kusahau Footwork yake nzuri kabisa.

Kwa staili yake ya uchezaji tutegemee wapinzani kulaumiana sana kwa kushindwa kumkaba Mayele.

Hii ni sawa kusema kuwa washambuliaji wengine wa Yanga wana mlima mrefu wa kuupanda ili kuweza kuanza badala yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live