Zikiwa zimepita siku chache tangu uenee uvumi wa uwepo wa Mchezaji wa zamani wa Yanga SC (kwasasa akiwa Pyramids FC) Fiston Mayele kuwa ndani ya Dar es Salaam, Hajis Manara ameandika na kutoa sifa kwa mchezaji huyo akidai kuwa hakuna mchezaji wa kigeni namba 9 mkali kuliko Mayele kati ya wote waliocheza Ligi Kuu ya Tanzania.
Manara amemalizia andiko hilo kwa kusema kuwa hakuna aijuaye kesho, na kuwafanya baadhi ya watu kuamini kuwa kuna uwezekano striker huyo wa Kimataifa kutokea Congo akarudi nyumbani Jangwani.
"Pengine nilikuwa sijaeleweka kwa walio wengi kipindi kile, nilishasema mara kadhaa na naendelea kuamini hivyo hadi sasa,Tanzania haijawahi kuintroduce Namba Tisa bora zaidi wa kigeni katika ligi yetu kumzidi Fiston Mayele.
"Ni Striker aliyejaaliwa kila kitu uwanjani na hakuna hata mtu mmoja atasema mapungufu yake ndani ya uwanja, kuanzia kufunga, kuasist, nguvu, control, mipira ya kichwa, mashuti, kufunga ndani na nje ya box na hata nidhamu yake kiwanjani.
"Ni Bugati Mtupu, full package, anakuofer kila kitu kama Namba Nine, ni vile tu maisha yanaenda ilivyopangwa tu, lakini nani ajuae kesho?" amesema Manara.