Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele anapiga kamba tu, anakitaka kiatu EPL

Timu Ya Mayele Yatolewa Nusu Fainali.jpeg Mayele anapiga kamba tu, anakitaka kiatu EPL

Fri, 15 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa mshambuliaji wa Timu ya Yanga ambaye kwa sasa anakipiga Pyramids FC ya Misri, Fiston Kalala Mayele amefunga bao lake la nne ndani ya Ligi Kuu ya Misri (EPL) akiwa na uzi wa timu yake hiyo mpya.

Mayele ambaye msimu uliopita ndiye alikuwa Kinara wa upachikaji mabao katika Ligi Kuu ya NBC nchini Tanzania, kwa sasa anazidiwa mabao mawili na kinara wa upachikaji mabao ndani ya Ligi Kuu ya Egypt msimu huuu.

Mayele alifunga bao la kuongoza la timu yake dhidi ya Baladeyet El Mahalla FC dakika ya 22 hapo jana kabla ya timu hiyo kusawadhisha kupitia kwa Hossam Ashraf dakika 10 baadaye.

Kipindi cha pili, Pyramids walipata bao kupitia kwa Fagrie Lakay dakika ya 46 kabla ya Mahalla kusawadhisha dakika ya 75. Mayele alifunga bao jingine lakini VAR ililikataa bao hilo na mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 2-2.

Pyramids FC ndiyo wanaongoza Ligi Kuu ya Misri wakiwa na alama 17 katika michezo 8 waliocheza wakati Al Ahly ambaye ni Bingwa mtetezi akiwa na alama 16 kwenye michezo 6 aliyocheza mpaka sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live