Fiston Kalala Mayele ni kama alianza kujichimbia kaburi yeye mwenyewe kupitia maneno yake lakini tu alikuwa hajajaa kwenye mfumo wa Watanzania sasa ni rasmi kajaa kupitia kauli zake.
Mayele ni moja ya wachezaji ambao wanacheza sana kwenye mitandao kuliko uwanjani kwa siku hizi na anachokifanya huwa si fair play bali hufanya dharau kwa wengine kupitia mitandao yake.
Mara kadhaa alirusha tuhuma zisizo za kweli kwa Mamelodi Sundowns kwamba walitengeneza hila ili anyimwe VISA ya kuingia Afrika Kusini kwenye mchezo wa CAFCL dhidi ya timu hiyo uliofanyika mwaka Jana pasipo yeye kuwepo.
Aliwahi kusema AZAM FC wanakamia mechi moja kauli mbovu ambayo imewahi kutolewa na mchezaji professional kama yeye ni hii pia alishindwa kuuheshimu wanachokifanya na kuvuja Jasho wapinzani wake wakiwa uwanjani.
Leo anakuja na hoja kuwa amechoka kutumiwa majini na viongozi wa Yanga timu ambayo imemtoa kwenye soka lake kimataifa leo anaigeuka na anatoa shutuma kama zile alizowahi kutumia kwa Mamelodi Sundowns.
Mayele aliisema kwenye michuano ya AFCON iliyotamaika juzi, Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kuwa ilikamia mchezo wao dhidi ya Congo DR na kutumia mabeki watano ili wasifungwe.
Ukweli ni kwamba alianza kujichimbia kaburi yeye mwenyewe sema tu alikuwa hajashtukia mchongo sasa Wabongo wameanza kumuwamba anakuja kuomba poo wakati mziki aliuwasha mwenyew.
Ukiwa professional fanya kama professional ila ukileta uswahili alafu unataka watu wakuine professional ni ngumu sana.
Mtazame Fiston Mayele amekuwa akiwekeza nguvu nyingi kwenye maneno zaidi tangu ajiunge Pyramids, kwenda kuandika kuwa watu wana chuki na yeye na alifanya kosa kucheza Tanzania.
Hii inaleta picha kwa kile alichokizungumza kocha wa Mamelodi Sundowns, Rhulani Mokwena kuwa hivi sasa Fiston Mayele anacheza mpira Twitter na Instagram.
Greenwood kuna wakati alitukanwa na kuwekewa chuki na mashabiki wa Manchester United, lakini hakuna mahali kwenye kurasa zake za mtandao aliandika kuwa chuki za nini na nilikosea kucheza Manchester United.
Mayele hivi sasa amewekeza kwenye siasa za football ya Bongo badala ya kuwekeza kwenye miguu yake aiache izungumze yenyewe.