Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele ampagawisha Kocha wa Club Africain

Aziz Ki X Mayele Aziz Ki na Fiston Mayele

Tue, 1 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Club Africain, Bertrand Marchand amesema moja ya staa wa Yanga anayemuhofia katika mchezo wa kesho wa mchujo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika ni Fiston Mayele.

Kwenye kikosi cha Yanga, Mayele ndiye kinara wa mabao kwenye Kombe la Afrika baada ya nyota huyo kutupia jumla ya mabao saba katika hatua zilizopita dhidi ya Zalan kutoka Sudan Kusini na Al Hilal ya Sudan.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Marchand amesema Mayele ni mchezaji mzuri ambaye anamfahamu kwa muda mrefu tangu akiitumikia AS Vita ya kwao DR Congo.

"Wakati nipo klabu nyingine kabla ya hii miaka miwili nyuma nilihitaji kumsajili kwa sababu alinivutia sana kutokana na aina ya uchezaji wake ila bahati mbaya sikufanikiwa kwa hilo." alisema Marchand.

Marchand aliongeza mbali na Mayele ila pia anawafahamu Tuisila Kisinda na Jesus Moloko japo Yanga ina wachezaji wazuri kutoka mataifa mbalimbali hivyo ni lazima wajiandae vizuri kutokana na ugumu wenyewe wa mchezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live