Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele amewaacha mbali Shalulile na Percy Tau - Ally Kamwe

Mayele Bora Mayele amewaacha mbali Shalulile na Percy Tau - Ally Kamwe

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Shabani Kamwe amesema kuwa tuzo ya CAF ya Mchezaji Bora wa Mwaka (Ligi ya Ndani) alipaswa apewe aliyekuwa mshambuliaji wa Timu hiyo, Fiston Mayele.

Kamwe amesema hayo baada ya tuzo hiyo kwenda kwa mshambuliaji wa Al Ahly raia wa Afrika Kusini, Percy Tau.

Ikumbukwe kuwa, Mayele ndiye aliisaidia timu yake kufika hatua ya fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika huku akimaliza kama mfungaji bora kwa kufunga jumla ya mabao 7.

"Ameshinda Percy Tau? Wapiga kura wanajua zaidi, lakini kwangu, sidhani kama kuna mchezaji ndani ya Bara la Afrika aliyekuwa kwenye kiwango bora kwa mwaka 2023 zaidi ya Fiston Mayele.

"Na ziko nyakati tunamuweka Mayele nyuma ya Peter Shalulile kwa sababu tu, Shalulile yuko Mamelod na ana baadhi ya medali kwenye shingo yake, lakini in terms ya wanachokitoa kwenye pitch, bado ntaondoka na Fiston Mayele bila kuwaza mara mbili.

"Predetor Fiston Mayele sio tu top three, alistahili kuondoka na Tuzo yake kabisa. Mwaka 2023 kafanya mabalaa mengi sana," amesema Ally Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live