Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele ameukosea mpira

Mayele Pyramids Hoi(2).jpeg Mayele ameukosea mpira

Wed, 14 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Didier Drogba aliwahi kusema "Football is more than just a game. It can bring hope and joy to people's lives."

Anamaanisha Football ni zaidi ya mchezo, inaleta matumaini na furaha kwenye maisha ya watu lakini pia naweza kuongezea sio furaha tu, mpira unauma na unaua.

Tunapozungumzia maisha ya watu, tunagusa feelings yaani hisia Football inaleta hisia zenye pande mbili tofauti kwa maana ya furaha isiyoelezeka na huzuni isiyozungumzika.

Ukiingia kwenye Football lazima ukubaliane na hizo pande zote mbili, bila hivyo utauchukia mpira zaidi ya kuibiwa mkeo.

Kaka yetu George Weah nae aliwahi kugusia kidogo akasema; "Football ni lugha ya ulimwengu wote. Inaleta watu pamoja, bila kujali mataifa, tamaduni au imani zao."

Tafsiri yake kwenye mpira hakuna Utaifa wala Kabila na ndio maana tabia za kibaguzi nk. zinapingwa duniani kote, lakini pia ndio maana mchezaji anaweza kucheza sehemu yeyote duniani na akajihisi yupo nyumbani.

Ndugu yetu Mayele umeukosea mpira kwa kushindwa kuhimili hisia za watu wa mpira na kushindwa kuishi kwenye dhana ya mpira unaileta dunia pamoja bila kujali utaifa, tamaduni au imani.

Kauli ya "au nilikosea kucheza timu za Tanzania" haina afya kwasababu Football ya nchi yoyote ina pande zote mbili (furaha & huzuni).

Huzuni na Furaha huwa zinaleta kauli nyingi za kukufurahisha na kukukera, wewe kama Professional Footballer lazima uelewe hilo na kazi yako kubwa ni kuacha miguu yako uliyobarikiwa na mwenyezi Mungu iongee.

Kujibizana na watu waliojaaliwa kipawa cha kuongea ni kukikosea kipaji chako, acha uwezo wako uongee.

Achana na Ronaldo na Messi ambao wanaongoza kupendwa na kuchukiwa hapa duniani, Simon Msuva ni darasa zuri kwako.

Kuna wakati alikuwa akiingia uwanjani mshabiki wa timu yake walikuwa hawampendi na kumtolea lugha mbaya ambazo kibinadam hazijakaa sawa na zinakatisha tamaa lakini alichagua kuacha miguu yake iongee.

Oh My God, Kila nikifikiria kuhusu Harry Maguire najisemea King Fiston Mayele ???????? cheza Mpira.

Unazungumza kuhusu Majini? Watu walitishiwa hadi kuuwawa. This is Football, hakuna namna ya kuzuia unachotaka kisizungumzwe juu yako, acha miguu izungumze.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: