Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele alikacha safari DR Congo kupambania kiatu Mbeya

Myele Vs Prisons Mbeya Mayele alikacha safari DR Congo kupambania kiatu Mbeya

Sat, 10 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele amesema kiungo wa Simba, Saido Ntibazonkiza alimpa changamoto baada ya kufunga mabao 5 katika mechi dhidi ya Polisi Tanzania na kumsongelea yeye akiwa na 16 hivyo alighairi kwenda kwenye kikosi cha timu ya taifa na kuwahi Mbeya kucheza mechi ya mwisho.

Mayele ameyasema hayo wakati akihojiwa na kituo cha Azam TV akiwa kwenye basi maalum la wazi ambalo wanalitumia kuonyesha kombe la ubingwa la 29 amesema ilikuwa mechi mbili za mwisho dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons asicheze ili kupumzika kwa ajili ya kujiandaa kimataifa.

"Kuna kipindi nilikuwa na 16 wale walikuwa nyuma yangu walikuwa na 10 na mimi nilikuwa bize na kimataifa , mwisho Saido akaleta changamoto nzuri na mimi nampongeza ni mchezaji mzuri nimecheza naye Yanga namfahamu na yeye ananijua nampongeza sana," amesema Mayele na kuongeza;

"Ilikuwa sapraizi kwasababu nilikuwa najiandaa niende timu ya Taifa hizi mechi mbili za Ligi sikutakiwa kucheza muda tunacheza na Mbeya City yeye na Polisi akafunga matano bwana nikakata tiketi nikaenda Mbeya kucheza mechi ya mwisho,"

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: