Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele akubali kumfuata Nabi Kazier Chiefs

Nabi Amtaka Mayele Kaizer Mayele akubali kumfuata Nabi Kazier Chiefs

Thu, 15 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika Kusini imeonesha nia ya kutaka huduma ya mshambuliaji wa Pyramids FC ya Misri, Fiston Kalala Mayele raia wa Congo DR.

Taarifa kutoka nchini Afrika Kusini zinasema kuwa, Mkurugenzi wa Kaizer Chiefs, Kaizer Junior amezengumza na uongozi wa Pyramids FC lakini kuhusu uwezekano wa kumnasa mshambuliaji huyo wakiweka dau la Randi milioni 15.

Itakumbukwa kuwa, Mayele amewahi kufanya kazi na Kocha Nasreddine Nabi raia wa Tunisa kwa mafanikio makubwa ndani ya Yanga katika misimu miwili kabla ya nabi kutimkia FAR Rabat ya Morocco na Mayele kwenda Pyramids.

Inaelezwa kuwa, Nabi amedhamiria kuinasa saini ya Mayele na kumshusha ndani ya viunga vya Naturena kwani anajua uwezo wake na Mayele anajua mbinu za kocha huyo hivyo ni rahisi kufanya kazi pamoja.

“Hakuna tatizo kwenye upande wa mchezaji lakini tatizo ni pesa ambayo kaizer wameweka. Kaizer hawataki kutoa pesa ambayo tumewaambia licha ya kwamba pesa wanazo, kwa hiyo maamuzi yako mikononi mwao,” amesema Meneja wa Mayele.

Itakumbukwa kuwa, hivi karibuni Kaizer Chiefs ilishushiwa kipigo kizito cha bao 4-0 na Yanga kwenye michuano ya Toyota Cup na Yanga kufanikiwa kuibuka mabingwa wa mashindano hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: