Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele akabidhiwa Prisons

MAYELE JERAHA SD Mayele akabidhiwa Prisons

Fri, 9 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ili kutimiza azma yao ya kumuwezesha Straika wake Fiston Mayele kutwaa tuzo ya mfungaji bora, Yanga imemuanzisha nyota huyo ambaye anapambana vikali na staa wa Simba, Saido Ntibazonkiza katika kinyang'anyiro hicho.

Mayele ndiye kinara hadi sasa kwa idadi ya mabao akiwa nayo 16 huku Ntibazonkiza akiwa ameweka 15 na timu hizo zitakuwa kazini baadaye kukipiga na wapinzani.

Yanga itawakabili Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya huku Wekundu wakiwa Dar es Salaam dhidi ya Coastal Union.

Katika mechi zilizopita, Yanga ilimkosa Mayele wakati wa sare ya mabao 3-3 dhidi ya Mbeya City huku Wekundu wakishinda 6-1 mbele ya Polisi Tanzania huku Saido akiweka wavuni mabao matano na kuwafanya Yanga kumuwahisha haraka staa wao kucheza mechi ya leo Mbeya.

Mbali na Mayele pia Yanga ilimkosa kipa wake Djigui Diara raia wa Mali ambapo leo ameanza pamoja na mastaa wengine.

Hata hivyo iwapo Mayele atafunga leo, atakuwa ameondoa gundu dhidi yake na Wajelajela hao kwani ni moja ya timu ambayo hajaifunga tangu kutua nchini.

Kikosi hiki hapa; Diara, Dickson Job, Joyce Lomalisa, Ibrahim Bacca, Bakari Mwamnyeto, Salum Aboubabakari, Zawadi Mauya, Tusila Kisinda, Mayele, Mudathir Yahya na Kennedy Musonda.

Benchi wapo Metacha Mnata, Kibwana Shomari, David Bryson, Denis Nkane, Mamadou Doumbia, Yannick Bangala, Dickson Ambundo, Aziz Ki na Clement Mzize.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: