Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mayele ajazwa minoti sio poa

Mayele Fiston Kalala Fiston Mayele

Fri, 23 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), ambayo ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara, NBC Premier League, imekabidhi zawadi ya pesa na tuzo kwa Mchezaji Bora wa ligi hiyo wa Novemba, Fiston Mayele, kutoka Klabu ya Yanga.

Makabidhiano ya zawadi hizo yalifanyika muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo kati ya Yanga na Coastal Union uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Jumanne wiki, mchezo ambao ulikamilika kwa timu yao kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Mabao ya Yanga katika mchezo huo mawili yalifungwa na Mayele na la tatu likizamishwa nyavuni na Feisal Salum 'Fei Toto'.

Katika tukio la makabidhiano ya zawadi hizo, lilishuhudiwa na Mjumbe wa Bodi ya Ligi, Azim Khan, ambapo Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Elvis Ndunguru, alikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja kwa mchezaji huyo wa Yanga pamoja na tuzo

Akizungumza baada ya kukabidhi zawadi hizo, Ndunguru alisema NBC itaendelea kutoa hamasa kwa wachezaji na makocha kwa kila mwezi ili kuleta ushindani kwa wachezaji na makocha wote wanaoshiriki ligi hiyo.

“Tuzo hizi za kila mwezi tunazitoa kwa kuleta hamasa kwa wachezaji na makocha wa kila timu zinazoshiriki Ligi Kuu ili wafanye vizuri na kujitangaza kimataifa, pia kusaidia kuboresha mchezo huu wa soka hapa nchini,” alisema Nduguru.

Pia, akifafanua zaidi mipango ya     

benki hiyo, alisema ni kuboresha udhamini wake ambapo wapo katika hatua za mwisho kuanza kutoa mikopo ya mabasi kwa klabu mbalimbali zinazoshiriki Ligi Kuu ili kuzirahisishia usafiri.

“Pia, NBC tunaendelea kudhamini michezo mingine zaidi hapa nchini kama riadha kupitia NBC Dodoma Marathon na mashindano ya mchezo wa gofu tukidhamini Klabu ya Lugalo , lengo letu ni kusaidia sekta ya michezo nchini kuwa na kiwango cha kimataifa na pia kuboresha maslahi ya wanamichezo kwa ujumla.“

Kwa upande wa Mayele, alishukuru kupatatuzo hiyo na kuahidi kuwa atazidi kuongeza bidii kuwa kinara katika timu yake na kusaidia kupata ushindi kila mechi.

“Napenda kuwashukuru NBC kwa kutoa tuzo hii, inaongeza sana hamasa kwa upande wangu na wa wachezaji wote na makocha pia, nawashukuru benchi la ufundi na wachezaji wenzangu kwa pamoja wameniwezesha kupata tuzo hii na nitazidi kufanya vizuri," alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live