Nyota wa klabu ya Yanga, Fiston Mayele hivi karibuni amekuwa gumzo kwa baadhi ya vyombo vya habari nchini Ufaransa, ambapo nyota huyo ameonekana katika kituo Cha Televisheni Cha “Canal Plus” akijadiliwa na wachambuzi wa soka nchini humo kama “El dorado in Tanzania” kwa maana ya mfalme wa dhahabu Tanzania.
Mjadala huo unakuja kufuatia Straika huyo wa Mabingwa wa Tanzania Bara ambaye ni Raia wa Congo kuhojiwa na kituo hicho baada ya kufunga mabao 6 katika mechi mbili za Ligi ya Mabingwa alivyowafunga Zalan FC huku Yanga ikishinda bao 9-0 kwa mechi zote mbili.
Mayele ndiye mfungaji Bora wa Yanga msimu uliopita akiwa na mabao 16, huku akiwa mfungaji Bora wa pili wa Ligi.
Kwa msimu mpaka sasa Mayele anaongoza kwa mabao ndani ya Yanga akiwa na mabao 3 sawa na Feisal Salum kwenye Ligi ya NBC wakati kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika akifunga mabao 7 katika mechi tatu.